Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, Katika mikusanyiko mikubwa kama matembezi ya Arubaini, maandamano ya wananchi na mikutano mikubwa ya kijamii, mara nyingine swala ya jamaa huswaliwa kwa uongozi wa mtu asiyefahamika vizuri, na hivyo haiwezekani kuchunguza kwa undani uadilifu wake, katika hali kama hizi, swali linajitokeza: je, kuonekana kwa sura ya ucha Mungu wa dhahiri (kama vile kuvaa mavazi ya kielimu au mwenendo mwema) kunatosha kuhalalisha kumfuata Imamu huyo au la? Mtukufu Ayatullah Khamenei ametoa jibu la kisheria kwa istiftaa hii, ambalo tunaliwasilisha kama ifuatavyo.
Swali:
Katika hafla za umma kama matembezi ya Arubaini au maandamano, wakati mwingine mtu asiyejulikana kwa watu (kama vile mwanafunzi wa Hawza au sheikh) husimama kama Imamu wa jamaa, na hakuna nafasi ya kuchunguza uadilifu wake. Je, katika hali hii, iwapo mtu anaonekana kuwa na dini na mwema kwa dhahiri, je, hiyo inatosha ili Swala ya jamaa iwe sahihi?
Jibu la Mtukufu Ayatullah Khamenei (Mola amuhifadhi):
Katika kuthibitisha uadilifu wa Imamu wa jamaa, husnu al-zāhir (muonekano wa dhahiri) unatosha; yaani, iwapo mwenendo na tabia ya mtu huyo ni kwa mujibu wa masharti ya kisheria na hakuna dhambi inayoonekana kwake, basi watu wanaweza kuswali nyuma yake, na jukumu la kulitambua hilo ni la mwenyewe (mukallaf).
Vilevile, iwapo kwa sababu ya watu wengi kumfuata Imamu huyo wa jamaa ikapatikana yakini (yaani imani na utulivu wa nafsi kuhusu uhalali wake), hiyo pia inatosha.
Maoni yako